Privacy Policy
Taarifa tunazokusanya
Jina lako, namba ya simu na WhatsApp, jina la ofisi au duka, mahali pa kupeleka chakula, maelezo ya oda na kumbukumbu ya malipo unayotuandikia.
Kwa nini tunazitumia
Kuandaa na kuwasilisha oda yako, kuthibitisha malipo, kukupigia simu pale inapohitajika, na kushughulikia malalamiko. Hatuuzi wala hatukodishi taarifa zako kwa mtu yeyote.
Nani anaziona
Ni wafanyakazi wa Farzanah Foods pekee wenye kazi inayohitaji taarifa hizo — jikoni wanaona chakula kinachotakiwa, dereva anaona mahali na mpokeaji, na uongozi unaona taarifa za malipo.
Muda wa kuhifadhi
Kumbukumbu za oda na malipo huhifadhiwa kwa ajili ya hesabu za biashara. Unaweza kuomba tuondoe taarifa zako binafsi zisizohitajika kwa hesabu.
Mawasiliano
Kwa swali lolote kuhusu faragha, tuandikie info@farzanahfoods.com.